Serikali yaahidi kuutunza msitu wa Baba wa Taifa


Ofisi ya Waziri Mkuu, imesema itaanza kuusimamia na kuutunza msitu wa baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, uliopo Butiama, Mara kama sehemu ya kumuenzi na kuendelea kutunza mazingira.

 Hayo yamesemwa leo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katika kongamano la mazingira lililofanywa wilayani humo kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya mazingira duniani, yaliyofanyika kitaifa, wilayani Butiama.

“Sisi tutauangalia msitu huu, lakini tunaomba ushirikiano wa wakazi wa Butiama, tukiwaomba wiki hii mfanye kitu hiki, mtusaidie na tushirikiane,” amesema Makamu wa Rais

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com