Rais Magufuli: Wauaji Kibiti, Rufiji waombewe waokoke


Rais John Magufuli amewataka Watanzania wawaombee wanaofanya mauaji mkoani Pwani, waokoke ili wajue kuwa damu ya mtu ina thamani kubwa.

 Ameyasema hayo leo (Jumanne) wakati akihutubia katika mkutano wake wa kwanza katika ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani.

“Niwaombe wananchi wa Pwani, msishirikiane na watu waovu, wanachelewesha maendeleo. Ndiyo maana huko Kibiti hata viwanda hakuna, hakuna imani ya dini inayosema watu kuuana,” amesema.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano si ya kuchezea kwa sababu mpaka sasa wauaji hao wameshaanza kuuona moto.

 “Watanyooka, actualy wameshaanza kunyooka, kama wapo hapa wanaotusikiliza,  wakapeleke salamu,” amesema na kuongeza;

“Niwaombe sana, tuwaombee hawa watu waokoke, ili wajue damu ya mtu ina thamani kubwa.”


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com