Polisi: Hatuna Sheria ya Viboko kwa Madereva Wazembe

Kaimu Kamanda Mkuu wa kikosi Cha Trafiki Tanzania, SACP Fortunatus Musilimu amekanusha kauli ya Naibu waziri wa mambo ya ndani Hamad Masauni kuhusu adhabu ya viboko kwa madereva na kusema alimaanisha adhabu kali sana itolewe kwa madereva wazembe.

Kamanda Musilimu amesema kwamba kama jeshi la polisi, ulinzi na usalama barabarani hawataweza kuendelea kushuhudia ajali nyingi zikiendelea barabarani kutokana na madereva wazembe, hivyo watahakikisha maadhamio waliyoyapanga yanatekelezwa kwa asilia zote.

"Tutakuwa wakali sana kwa madereva wazembe, Hatutawachapa kwa viboko maana hakuna sheria inayosema hivyo. Lakini adhabu tutakazokuwa tukizitoa ni sawa na adhabu ya viboko. Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wa Mambo ya Ndani Massauni alisema inabidi kuchukua hatua kali dhidi ya madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani, ikibidi hata kuwachapa viboko akimaanisha adhabu na sivyo kama watu walivyomnukuu", Musilimu alifafanua

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com