PICHA 17: Real Madrid walivyowasili Hispania na Kombe

Usiku wa June 3 2017 katika uwanja wa Millenium jiji la Cardiff nchini Wales Real Madrid waliandika historia mpya katika uwanja huo baada ya kufanikiwa kutwaa taji lao la 12 la UEFA Champions League katika historia ya club yao.
Real Madrid walitwaa taji hilo baada ya kufanikiwa kuifunga Juventus ya Italia kwa jumla ya magoli 4-1, baada ya ushindi huo wa Real Madrid leo June 4 wamewasili nyumbani kwao Hispania na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wao.
Baada ya kuwasili Hispania Real Madrid walikaribishwa katika ukumbi wa City Hall jijini Madrid na baadae kutoka nje kuwasalimia maelfu ya mashabiki wao waliyojitokeza kufurahia ushindi huo, sherehe za Ubingwa wa Madrid zinaendelea usiku wa leo katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu.
Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos akimkabidhi Kombe la UEFA Rais wa jiji la Madrid Cristina Cifuentes
Mashabiki waliyokuwa wamejitokeza kwa nje
Sergio Ramos akimkabidhi jezi Cristina Cifuentes inayooneshwa wametwaa taji la UEFA kwa mara ya 12.
Cristina Cifuentes na Sergio Ramos
Cristina Cifuentes na Rais wa Club ya Real Madrid Florentino Perez
Cristina Cifuentes, Sergio Ramos na Rais wa Club ya Real Madrid Perez
Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos baada ya kumkabidhi jezi Meya Manuela Carmena


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com