Mwigulu: “Naelekeza wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya nchi yetu"

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa taarifa ya kumpongeza Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa uamuzi aliochukua baada ya kupokea ripoti ya pili ya mchanga wa madini.
Pamoja na pongezi, Waziri Nchemba ametoa maagizo kuwa watu wote waliotajwa kwenye ripoti hiyo wasiruhusiwe kutoka nje ya nchi isipokuwa kwa ruhusa maalum kutoka serikalini na kuvitaka vyombo vya usalama kuhakikisha vinasimamia agizo hilo.
“Hakuna uzalendo zaidi ya kulinda rasilimali za Taifa, Hakuna utetezi wa wanyonge zaidi ya kulinda rasilimali zao.Hongera sana Mh.Rais kwa uzalendo wa vitendo kwa Taifa letu.”
“Naelekeza wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini. Vyombo vitekeleze maagizo ya Rais kwa utimamu,” imesema sehemu ya taarifa ya Mwigulu Nchemba.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com