Mtoto wa Rais Karume ahamia CUF

Mtoto wa Rais wa Kwanza wa  Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume juzi alikiaga rasmi chama cha CCM na kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF) ambapo alipokelewa na kupewa kadi ya uanachama na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.
Halfa ya kukabidhiwa kadi ya chama ilifanyikia nyumbani kwa Maalim Seif Chukwani Zanzibar ambapo ilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Nassor Ahmed Mazrui.
Ikiwa sasa ni takribani siku tatu zimepita tangu Akhsa Abeid Aman Karume alipojiunga rasmi na chama hicho upinzani, amesema kuwa ana mengi ya kuzungumza lakini anasubiri kwanza mwezi mtukufu wa Ramadhani upite.
Wakati Akhsa akiyasema hayo, uongozi wa CUF visiwani humo umesema kuwa kuna viongozi wengine 12 kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) watakaojiunga CUF karibuni.
Akizungumzia suala la mtoto wa Rais Karume kujiunga CUF, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Salim Bimani amesema kuwa inaonyesha wazi kuwa chama hicho kinakubalika Zanzibar na kwa watanzania wote. Alisema kuwa wanachama wengi wa CCM bado wanachuki na chama hicho kufuatia kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa 2015 na kadiri siku zinavyokwenda watazidi kuhama.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com