Msukuma: Nina majina ya Wabunge Waliohongwa kutetea Mchanga wa Madini

Kwa kipindi kifupi kilichopita bunge letu lilianza kurudi kwenye misingi ya kizalendo, ila tokea hii budget ya madini ianzwe kusomwa vijembe,majigambo,maneno ya kuudhi,kejeli zimerejea mahali pake.

 kwa mara nyingine mbunge wa Geita, mh Msukuma aliomba dakika za nyongeza kutoka kwa Hawa Ghasia na kuwashambulia wabunge wa upinzani badala ya kuzungumza hoja. 

Mh. Msukuma alisema wapinzani wamehongwa na anawajua ingawa hakuwataja, pia akasema Msigwa anamiliki nyanya,kuku na mbwa hawezi jua mambo ya madini kama vile haitoshi akamrudia Mnyika kwamba anamiliki mchanga wa matofali.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com