Mkurugenzi wa haki za Binadamu kukamatwa na Polisi, Wadau wamlilia

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRD), wamelaani vikali kitendo cha kukamatwa kwa mratibu wa kitaifa wa mtandao huo Onesmo Ole Ngurumwa.

Tamko hilo limetolewa leo Jumamosi na mwanasheria wa THRD, Deogratius Bwire baada ya kukamatwa kwa mratibu huyo katika hoteli ya Blue Peal saa tatu asubuhi wakiwa wanajiandaa kuingia kwenye uzinduzi wa kitabu cha 'sauti ya watetezi wa haki vyuoni '.

Bwire amesema mpaka sasa hakuna taarifa rasmi za kukamatwa kwao baada ya ya wakili Jones Semdodo aliyoko kituo cha polisi cha magomeni kusema hakuna makosa yaliyoainishwa na wanasubiri maelezo kutoka juu.

Amesema Serikali na vyombo vya dola zifanye shughuli zao kihalali pasi na kuonea watu ambao wanafanya shughuli zao kihalali.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com