Mjane atishiwa maisha na watendaji wa Serikali

Mjane aliyefahamika kwa jina la  Bi. Modesta Mukurasi anayemiliki shamba la urithi lililonunuliwa na wazazi wake ameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi kati yake na watendaji wa serikali ya kijiji cha Bushumba wanaomtishia maisha yake.

Bi. Modesta anasema watendaji hao wamekuwa wakimpa vitisho kuwa watamuua endapo ataendelea kufuatilia na kudai shamba lake hilo ambalo inasemekana lina ukubwa wa ekari zaidi ya 30 ambalo kwa sasa limeuzwa kwa wawekezaji kinyemela. 

Mjane huyo amesema hayo katika kikao cha viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), watendaji wa serikali wilaya ya Muleba katika ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa, Ndugu Abdallah Bulembo iliyolenga kufafanua mabadiliko ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi na kutoa shukrani kwa wananchi kwa kumchagua Rais Dkt John Pombe Magufuli kuiongoza nchi.

Kutokana na malalamiko hayo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa Chama cha mapinduzi Mhe. Alhaj Abdallah Bulembo amelazimika kumkabidhi kwa uongozi wa serikali ya wilaya ya Muleba mama huyo ili asaidiwe kupata haki yake.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com