Meya apanda Basi la Abiria kwenda Kwenye Mazishi ya Ndesamburo


NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo ameondoka jijini hapa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa kutumia usafiri wa basi kuhudhuria mazishi ya Mbunge wa zamani wa Jimbo la Moshi mjini na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Mzee Philemon Ndesamburo aliyefariki dunia wiki iliyopita.

Meya Mwita ameondoka kwa kutumia usafiri wa basi baada ya gari lake kupata ajali na kuharibika vibaya Jumapili ya wiki iliyopita alipokuwa akitokea Dodoma kwenye kikao.

Akizungumza mara baada ya kuondoka katika stendi kuu ya mabasi ya Ubungo, Meya Mwita alisema kuwa msiba wa mzee Ndesamburo ni pigo kwa Taifa, Chama, wakazi na wananchi wote wa mkoa wa Kilimanjo  kutokana na ushawishi mkubwa aliokuwanao katika mkoa huo.

Mbali na hivyo alisema kuwa imekuwa nipigo kubwa pia hata ndani ya Chama kwa kuwa bado alikuwa akihitajika kutokana na busara na hekima alizokuwa nazo enzi ya uhai wake licha yakuwa alikuwa amestaafu nafasi ya ubunge kwenye jimbo hilo.

Wakati shughuli za kuaga mwili wa mzee Ndesamburo zikiendelea leo mjini Moshi katika viwanja vya Majengo, Meya Mwita anatarajiwa kufika mnamo saa 10 jioni ambapo ataungana na viongozi mbalimbali wa chama ngazi ya Taifa, Mikoa, wabunge na familia ya mzee Ndesamburo pamoja na
viongozi mbalimbali watakaoshiriki kwenye msiba huo.

Aidha anatarajiwa kurejea jijini hapa Jumatano wiki hii baada ya kumalizika kwa shuguli za mazishi hapo kesho.

Mzee Ndesamburo alifariki dunia Mei 31 mwaka huu akiwa njiani kupelekwa hospital ya Rufaa ya KCMC baada ya kupoteza nguvu  mwilini na atazikwa kijijini kwake Mbokomu kesho.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com