Manara atuma salamu za pole Yanga kwa msiba wa Ally Yanga

Mabingwa wa soka Tanzania bara kwa mara tatu mfululizo klabu ya Yanga wamepatwa na msiba mzito baada ya moja ya aliyekuwa mshabiki wao nguli kufariki.

Ally Yanga kama anavyofahamika amefariki hii leo mchana jijini Dodoma ambako taarifa zinasema alikuwa kwenye shughuli za kukimbiza mwenge.

Yanga alikuwa maarufu sana katika ushangiliaji kutokana na aina yake ya kipekee ya kujipaka mkaa usoni na kujaza nguo katika tumbo lake kama ana kitambi.

Kutokana na msiba huo aliyekuwa msemaji wa klabu ya Simba bwana Haji Manara ametuma salamu za pole kwa watani wake hao na akisema amehuzunishwa na msiba huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika “nimepigiwa simu kwamba Ally Yanga amefariki huko Mpwapwa mkoani Dodoma,msiba huu ni wetu wote na tunawapa pole watani zetu.”


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com