Lowassa Kuhojiwa na Polisi Kesho, Atumiwa Ujumbe na DCI


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameitwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Boaz.

Lowassa akizungumza na gazeti la Mwananchi leo (Jumatatu), amesema ameitwa kwa DCI lakini hajui anachoitiwa.

Hata hivyo, amesema anahisi ni kauli yake kuhusu mashehe wa kikundi cha Uamsho cha Zanzibar wanaoshtakiwa kwa tuhuma ya ugaidi.

 “Ni kweli nimetakiwa niripoti kesho saa 4:00 asubuhi katika ofisi ya DCI. Sijui wananiitia nini, lakini nahisi ni kuhusu nilichosema kuhusu mashehe wa Uamsho,” amesema Lowassa.

Jana katika taarifa kwa vyombo vya habari, Lowassa alikaririwa akimtaka Rais John Magufuli kuwaachia huru mashehe hao wanaoshikiliwa kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Taarifa hiyo ilisema Lowassa alitoa ombi hilo alipozungumza katika futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com