Kivuko MV Kazi chazinduliwa DSM, Kina uwezo wa kubeba abiria 800

Serikali imeendelea na juhudi zake za kuboresha huduma za kusafirisha magari na abiria kati ya eneo la magogoni na kigamboni jijini Dar es salaam, baada ya leo kupokea kivuko kipya chenye uwezo wa kubeba abiria mia nane (800).
Kivuko kipya kiitwacho MV KAZI kilichotengenezwa na Kampuni ya kizalendo kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilion 7.3 kinakuwa kivuko cha tatu kinachotoa huduma kati ya Kigamboni na Katikati ya jiji la Dar es salaam kikiwa na uwezo wa kubeba tani 170 na magari madogo 22.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof MAKAME MBARAWA amepokea kivuko hicho na kueleza kuwa serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha inaboresha pia vivuko vya Pangani na busisi ili kuwarahishia huduma za usafiri wananchi wa maeneo mbalimbali wanaotegemea vivuko .


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com