Gwajima atinga Moshi kumuaga Ndesamburo


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewasili katika viwanja vya Majengo, Moshi kwa ajili ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Chadema, Phillemon Ndesamburo.

 Tayari mwili wa Ndesamburo umewasili katika viwanja vya Majengo na kupokelewa na baadhi ya viongozi wa Chadema.

Mwili wa Ndesamburo ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini,utaagwa katika viwanja hivyo na leo saa 10 jioni utapelekwa nyumbani kwake kwa ajili ya taratibu za mazishi.

 Wabunge na Viongozi mbalimbali wa Chadema, akiwamo muasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, Frederick Sumaye wapo uwanjani hapo kwa ajili ya kumuaga Ndesamburo

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com