Familia yaendelea Kutia Mgomo wa Kuchukua Maiti ya Aliyeuawa na Polisi

Mvutano baina ya Familia ya Marehemu Salim Mohamed Almas aliyeuawa may 14 mwaka huu na Polisi katika eneo la Kurasini kwa tuhuma za Ujambazi kwa madai ya kutaka kupora fedha katika ATM umeendelea kuchukua sura Mpya ambapo familia ya marehemu imesema haitouchukua mwili huo na Kuuzika mpaka pale serikali itakapo unda tume huru kuchunguza mauaji yaliyotokea.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini dsm Msemaji wa familia hiyo ambaye pia ni mjomba wa marehemu Tulleyha Mohamed Abdulrahman amesema tume hiyo huru itakayoundwa itaweza kuondoa utata wa kifo hicho, ambacho wanadai marehemu Salim Mohamed Almas hakuwahi kujihusisha na Uhalifu na alikuwa mwanafunzi katika chuo Kikuu dsm kitengo cha IT.
Aidha amesema kutokana na kugubikwa kwa utata wa tukio hilo , walichukua hatua mbalimbali ikiwemo kuandika barua na kupeleka tume ya haki za binadamu,makao makuu ya jeshi la Polisi,ofisi ya rais ambapo pia wamekipongeza kituo cha haki za binadamu kwa kutoa ripoti ya Uchunguzi wa awali ambayo inadaiwa kuonyesha kuwapo kwa utata katika tukio hilo.
May 15 mwaka huu polisi katika eneo la kurasini wanadaiwa kumpiga risasi Salim Mohamed Almas kwa madai kuwa alikuwa akitaka kupora Fedha zilizokuwa zikipelekwa katika ATM iliyopo kurasini makao makuu ya uhamiaji,ambapo jeshi la polisi lilidai kuwa vijana wengine watatu walitoroka katika tukio hilo.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com