Ebitoke: Nimemuahidi Ben Pol Kumpa Kitu Chochote Anachokitaka (Picha + Video)


Siku chache baada ya Ben Pol na mchekeshaji anayekuja kwa kasi Bongo, Ebitoke ku-make headlines baada ya kukutana na kupiga picha zinazowaonesha wakiwa kimahaba, ikiwa ni baada ya mwanadada huyo kulalama kwa siku nyingi kwamba anampenda msanii huyo wa Bongo Fleva, Global  TV Online imemtafuta Ebitoke na kufanya naye mahojiano.


Katika mahojiano hayo, Ebitoke alisema kwamba watu wengi wanadhani kwamba ni kiki lakini kiukweli amefurahi sana kukutana na Ben Pol na kupiga naye picha pamoja na kupata nafasi ya kumueleza hisia zake live.


Ebitoke amesema hawezi kueleza nini kitafuatia kati yake na Ben Pol lakini amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa sababu ni kweli anampenda kwa dhati na yuko tayari kumpa chochote.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com