Daktari mbaroni kwa kuzaa na Watu 60

Mahakama moja nchini Uholanzi imeidhinisha ombi la familia zinazotaka vipimo vya vinasaba DNA vichukuliwe juu ya mmiliki wa kliniki ya uzazi ya daktari anayeshutumiwa kutumia mbegu zake za kiume katika makumi kadhaa ya kesi.

Jan Karbaat anashukiwa kuwa baba wa watoto wapatao 60 katika kituo cha afya alichomiliki katika eneo la Bijdorp, karibu na Rotterdam.

Vipimo sasa vitafanyika juu ya vifaa vilivyochukuliwa kutoka kwenye nyumba yake baada ya kifo chake mwezi Aprili, akiwa na umri wa miaka 89.

Wakili wa familia yake anasema hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai hayo.

Jan Karbaat alijiita "muasisi wa fani ya uzazi wa kusaidiwa".

Kliniki yake ilifungwa mwaka 2009 wakati kulikuwa na taarifa kwamba alidaiwa kugushi data, uchunguzi na maelezo ya watoaji wa mbegu za kiumena kuzidisha idadi inayoruhusiwa ya idadi ya watoto sita kwa kila anayejitolea kutoa mbegu za uzazi.

Katika kesi ya mahakamani mwezi uliopita, wakili wa wazazi 22 na watoto walisema kwamba visa vinavyoshukiwa vinajumuisha mtoto wa mteja wao mwenye macho ya hudhurungi wakati alikuwa na macho ya blu na mvulana wa mteja wakeambaye anasura inayofanana na daktari.

Taarifa za vinasaba DNA zitasalia kuwa siri hadi pale watoto watakapoonyesha kuwa kuna sababu za kuamini daktari alikuwa baba yao, kulingana na mwandishi wa BBC Anna Holligan, ambaye alikuwa katika mahakama ya wilaya ya Rotterdam.

Hatimae, kama taarifa za vinasaba-DNA zitawiana na watoto hao ambao wengi wao walizaliwa miaka ya 1980s, kutakuwa na tumaini la kumshitaki daktari, labda kwa misingi ya kwamba hawangepaswa kuwepo, ameongeza Anna Holligan

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com