BAVICHA Wamcharukia Spika baada ya Kumtoa Mnyika Bungeni mkukumkuku


Dar es Salaam. Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), limeaalani  kitendo cha udhalilishaji kilichofanywa na  Spika wa Bunge, Job Ndugai cha kumtoa kwa nguvu jana Waziri Kivuli wa Wizara ya Madini na Nishati, John Mnyika.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi na Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi wakati akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya chama hicho Kinondoni.

Katambi amesema Ndugai hakutumia busara kumtoa Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Kibamba, bali alikuwa na jazba katika kutoa uamuzi huo wa mbunge.

“Adhabu ya Mnyika kutoka nje ya Bunge ilitosha kabisa. Lakini si kumwambia asihudhurie vikao  kwa siku kadhaa,” amesema Katambi.

Amesema ni wakati mwafaka wa Ndugai kufanya upya marejeo ya uamuzi aliyoutoa ambao kwa anadai ulikuwa wa jazba kuliko busara.

Hata hivyo, Katambi amesema vita ya madini haiwezi kufanikiwa kwa kuwatoa  wapinzani nje ya Bunge ambao wana mawazo mbadala ambayo yanaweza kuwasaidia kwa namna moja au nyingine.

“Tunasikitika na kitendo kilichofanywa na Ndugai, nadhani busara alizisahau nyumbani basi angejaribu hata kuzikumbuka kuliko kutoa uamuzi kama ule."


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com