Baba afumwa na Mwanafunzi Iringa, Angalia Kilichotokea

AMA kweli za mwizi arobaini! Ndicho kilichomtokea mbaba anayefanya biashara ya kitimoto maeneo ya Kihesa, Kilolo mjini Iringa, Katito Nganga (35), baada ya kufumaniwa akivunja amri ya sita na denti wa kidato cha kwanza (jina na shule vinahifadhiwa) katika kipindi ambacho Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ amekataza wanafunzi wanaopata mimba kuendelea na masomo.

Hatua ya kukamatwa kwa mbaba huyo ilikuja huku serikali ikiwa imetoa onyo kwa mwanaume ambaye atakutwa na mwanafunzi katika maeneo tata au akifanya naye mapenzi ambapo atakamatwa na kufikishwa mahakamani kisha adhabu yake ni kwenda jela miaka 30.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mbaba huyo alikutwa na mkasa huo wikiendi iliyopita majira ya saa 5:00 usiku akiwa ndani ya chumba cha mwanafunzi huyo nyumbani kwa wazazi wake akiendelea kuigaragaza amri ya sita.

Ilidaiwa kwamba, kwa muda mrefu mbaba huyo alikuwa akimdanganya na kumhadaa kuwa, atamuoa na kuwa mke wake wa pili ili auze klabu ya pombe za kienyeji ya baba’ke.

“Baada ya kujiridhisha, tuliweka mtego baada ya kuona nyendo za mwanafunzi huyo si zenyewe na siku hiyo, kama kawaida yake, Nganga aliingia chumbani kwa mwanafunzi huyo na kuendelea na mambo yake.

“Hapo ndipo tulipoita polisi na kumkamata kisha kwenda kuwekwa mahabusu kusubiri sheria ichukue mkondo wake,” alisema mmoja wa mashuhuda hao ambaye ni ndugu wa mwanafunzi huyo aliyeomba hifadhi ya jina.

Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP John Kauga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi kwa upelelezi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani.

STORI: FRANCIS GODWIN, IRINGAJIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com