AUDIO: Kinachoendelea baada ya moto Kuunguza Bweni la Wasichana Mbalatse Sekondari Makete

Siku chache baada ya bweni la wasichana shule ya sekondari Mbalatse wilayani Makete mkoani Njombe kuunguzwa na moto, uongozi wa shule hiyo bado unaendelea na jitihada zake za kuhakikisha bweni hilo linarejea katika hali yake ya kawaida

Hatua hiyo itasaidia wanafunzi kuendelea kutumia bweni lao badala ya kulala madarasani kama ilivyo sasa ikizingatiwa kuwa bado wiki chache shule iweze kufunguliwa baada ya likizo kumalizika

Akizungumza kupitia kituo cha redio Green Fm Shuleni hapo hii leo makamu Mkuu wa shule hiyo Mwl. Yohana Pilla  amesema licha ya changamoto ya moto uliounguza vifaa vya wanafunzi hao Juni 16 mwaka huu, wameendelea kuwatia moyo wanafunzi hao na kubainisha kuwa mpaka sasa wanaendelea vizuri baada ya tukio hilo

Aidha mwalimu huyo amewaomba wananchi kwa kadri watakavyojaliwa kuisaidia shule hiyo kwa hali na mali kwa kuwa hivi sasa wanatakiwa kupata vitu vipya vya wanafunzi baada ya baadhi kuunguzwa na moto yakiwemo magodoro


Usiku wa Juni 16 Mwaka huu bweni la wasichana katika shule hiyo ya sekondari liliwaka moto ambao mpaka sasa chanzo chake hakijajulikana moto ambao ulizimwa mapema kabla haujaleta madhara makubwa zaidi

Bonyeza play ya sauti hizo hapo chini umsikilize:-


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com