Zitto Kabwe asikitishwa na kitendo alichofanyiwa Adam Malima, atoa kauli

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zuberi Zitto Kabwe amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na moja ya askari polisi kumtishia bunduki aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima

Zitto kabwe ameonyesha masikitiko hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii Facebook akihoji kama polisi wanafundishwa kuwafanyia hivyo raia.

"Hii ni nini ?, askari wetu wanafundishwa kufanya hivi, Waziri Mwigulu huyu yupo wazi na ni wa kutoka kwako. Unahitaji uchunguzi". Ameandika Zitto


Zitto ameandika hayo baada ya masaa machache kupita kwa tukio hilo lililowahusisha askari hao walioambatana na kampuni ya Majembe Auction Mart waliokuwa wakitaka kujaribu kukamata gari iliyokuwa imeegeshwa pembeni ya barabara ya Masaki karibu na Hoteli ya Double tree ingawa ndani ya gari hilo alikuwepo dereva.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com