Wolper aikana Chadema kweupee!

Malkia wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper adai kuwa hajawahi kuwa Mwanachama wa Chadema huku akisema kuwa alikuwa ana msapoti aliyekuwa Waziri wa Zamani, Edward Lowassa na siyo chama hicho.

Wolper ameyasema hayo katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kwenye ukurasa wa facebook EATV.
“Mimi nilifanya siasa kwa sababu namheshimu Muheshimiwa Lowassa, na mimi ni shabiki wake na familia yake kwa ujumla. Nilianza kumsapoti Lowassa wakati yupo CCM. Mimi ni mfanyabiashara na muigizaji, sijawahi kuwa mwanasiasa ndio maana nilikuwa namsapoti mtu mmoja mmoja na siyo chama,” alisema Wolper.
“Hata hivyo mimi siyo Yuda kwa sababu sijawahi kuwa mwanachama wao na sina chama chochote lakini wao baada ya uchaguzi walinitelekeza kiasi cha kunifanya nijisikie mpweke. Hata kama hawakushinda uchaguzi walipaswa hata viongozi wawili wanishukuru tu kwa maneno ili na mimi nipate faraja lakini hawakuweza kufanya hivyo.”


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com