Wivu wa kimapenzi wasababisha kifo, Afyekwa Mguu

Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Sultani Ali Tani mwenye umri wa miaka 41 amefariki Dunia baada ya kuchinjwa na kisu katika mguu wake wa kushoto.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili za usiku maeneo ya kizimbani wete pemba.
Imeelezwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi ambapo Marehemu alikua na wake wawili wanaojulikana kwa majina ya Bi. Punje na Bi. Khadija.
Inadaiwa kuwa hapo Jana marehemu alikua na zamu ya kulala kwa Bi. Khadija lakini mpaka saa mbili usiku Marehemu alikua hajarudi ndipo Bi. Khadija alipotoka na kisu na kuelekea kwa mke mwenzie na alipomkuta mumewe huko alimkata na kisu kwenye mguu wake wa kushoto kulipopelekea Marehemu kupoteza damu nyingi na hatimae alipoteza maisha.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com