Wanatanzania changamkieni Fursa Hii - Asema Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewataka Watanzania kuchangamkia fursa kwenye mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale-Uganda hadi Tanga-Tanzania.
Rais Magufuli amesema mradi huo ni kielelezo tosha cha muendelezo wa ushirikiano wa nchi zetu mbili.
“Nchi yetu imepata mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale/Uganda hadi Tanga/Tanzania,ni fursa kubwa ktk kuujenga uchumi wetu. “Mradi huu ni kielelezo tosha cha muendelezo wa ushirikiano wa nchi zetu mbili na hasa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,” Rais Magufuli alitweet.
“Wito wangu kwa watanzania wote ni kuchangamkia fursa hii kipindi cha ujenzi na uendeshaji wa mradi huu. Mungu Ibariki Tanzania.”JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com