Waandishi waliokamatwa Arusha waachiwa huru

Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari mkoani Arusha wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kushiriki katika mkusanyiko usio halali walipokuwa wameenda kufanya kazi zao.
Mkusanyiko hiloulielezwa kuwa ulikuwa na lengo la kuwapa rambirambi wazazi waliofiwa na watoto katika ajali ya basi la Shule ya Msingi Lucky Vicent ya jijini Arusha.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo alisema mmoja kati ya viongozi wa Tamongsco, Kanda ya Kaskazini alikuwa na Sh milioni 18 kwa ajili ya kutoa rambirambi kwa wafiwa lakini ilishindikana baada ya kukamatwa na polisi waliofika shuleni hapo.
Waandishi waliokamatwa ni pamoja na Godfrey Thomas (Ayo Tv), Alphonce Kusaga (Triple A), Hussein Tuta (ITV), Joseph Ngilisho (Sunrise Radio), Filbert Rweimamu (Mwananchi), Janeth Mushi (Mtanzania), Elihuruma Yohani (Tanzania Daima) na Idd Uwesu (Azam Tv).
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ilembu alisema, waandishi hao walikamatwa kimakosa hivyo waliachiwa huru baada ya kutambulika.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com