Vitendo vya Rushwa, CCM Makete jino kwa Jino na Wanachama Leo

Wananchi  wilayani  Makete mkoa wa njombe wametakiwa kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa  kwa kuwa  vitendo hivyo ni kinyume cha sheria.

 Akizungumza katika mkutano na  viongozi wa chama cha mapinduzi wa kata ya tandala katibu mkuu wa chama hicho  wilaya ya Makete Bw. Lengae Godsoni Akyoo amesema vitendo vya rushwa havina budi kukemewa kwa nguvu zote.

Bw.Akyoo ameongeza kuwa kuelekea  katika uchaguzi  wa ndani ya chama hicho  vitendo vya rushwa hivitafumbiwa macho ili kuweza kupata viongozi  stahiki.

 Alexanda Mbilinyi ni mmoja ya  wajumbe waliohudhuria katika mkutano huo  naye anakiri kuwepo kwa vitendo  vya rushwa katika jamii na hasa nyakati za uchaguzi.

 Katika hatua nyingine mwenyekiti wa chama hicho  wilaya ya Makete  BW. FRANSIS CHAULA amesema ili kuimarisha demokrasia  mambo yote ya uchaguzi wa ndani ya chama hicho yanatakiwa kufanyika kwa uwazi.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com