Ukaguzi mzito wa mabasi yanayobeba Wanafunzi wafanyika mkoani Singida


 Baadhi ya mabasi kati ya 20 yanayotumika kusafirisha wanafunzi Mkoani Singida yakifanyiwa ugazi na askari usalama barabarani kwa lengo la kujiridhisha ubora wake.


Askari wa usalama barabarani mkoani Singida, E.8763. Sgt. Benes Lucas akikagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi mjini hapa jana.

Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani Mkoa wa Singida limeanzisha zoezi kambambe la kukagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi huku likisisitiza kuwa zoezi hilo kuwa endelevu.

Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida, RTO Mrakibu wa Polisi Peter Raphael Majira, amesema zoezi hilo lililoanza jana litaendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa Singida.

Amesema lengo ni kuhakikisha mabasi hayo yanakidhi mahitaji yote ya sheria za usalama barabani, wakati wote yanapokuwa barabarani.

Amesema pia wanatoa elimu na wanawakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo, juu ya wajibu wao na umuhimu wa kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani.


Aidha RTO Peter amesema wanawakumbusha madereva kujenga utamaduni wa kuwa na tahadhari zaidi na kitendo hicho kitapunguza kwa kiwango kikubwa ajali za barabarani.

Pia ametumia fursa hiyo kuwataka wenye watoto wanaotumia mabasi hayo wahakikishe mtoto anakaa kwenye kiti chake na si kuchangia kiti.

“Mzazi/mlezi usikubali kabisa mwanao achangie kiti, umelipitia kiti kwa nini achangie na wanafunzi mwingine. Na ninyi wamiliki wa mabasi haya kama kuna hafla wanafunzi wanakwenda kuhudhuria iwapo wamejaa (yaani kila mwanafunzi ana kiti chake), peleka hao waliopata viti halafu urudie wengine” amesisitiza mrakibu Peter.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com