Treni ya abiria Yapinduka Morogoro Usiku wa Kuamia leo

Taarifa fupi na picha kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeeleza kuwa treni ya abiria iliyokuwa ikienda bara imepata ajali saa 5:25 usiku eneo la stesheni ya Mazimbu Morogoro jana Ijumaa Mei 12. 

Mabehewa saba (7) yamehusika katika ajali hii manne (4) yakiwa yameegama na matatu (3) yameacha reli. 

Abiria moja ameumia baada ya kuangukiwa na mizigo na anaendelea na matibabu. 

Abiria wengine wanasubiri utaratibu wa kutafutiwa usafiri mbadala wa safari yao. 

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com