Simba SC tutatumia Dola Elfu 15, kuipeleka Barua FIFA – Aveva

Baada ya Kamati ya maadili na hadhi za wachezaji kuipoka klabu ya Simba SC alama tatu ilizopewa na kamati ya saa 72, rais wa klabu ya hiyo, Evans Aveva amezungumza na waandishi wa habari hii leo na kuelezea maamuzi ya klabu hiyo.
Aveva amesema Simba SC wanaonewa katika hilo na kamwe hawawezi kulikalia kimya swala hilo, na kwa sasa wanangoja barua ya maandishi kutoka kwenye bodi ya shirikiso la soka nchini, TFF, ili kulipeleka swala hilo kwenye shirikisho la soka duniani, FIFA pamoja na kulipeleka suala hilo katika mahakama ya michezo CAS.
Kuhusiana na maamuzi hayo yaliyotolewa na TFF kupitia kwa katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa, TFF walishasema Simba haiwezi kukata rufaa tena.
Wao kama Simba Sc wanaona alama tatu ni mali yao, na hivyo kuna mkanganyiko kati ya Bodi na kamati ya haki na hadhi za wachezaji, na kwao wanajua kadi tatu zilikuwepo kwa kuwa hakuna kamati hata moja inayopinga suala hilo.

Swala lingine ambalo Rais Aveva amelizungumzia ni juu ya mchezo wao wa fainali kati ya Simba Sc dhidi ya klabu ya Mbao Fc, na kusema kuwa wanaomba waendeshaji wa mashindano hayo pamoja na wadhamini wake kupewa heshima inayoambatana na mashindano kwa kuwa ni makubwa na yanatoa mshiriki wa kimataifa na hivyo kuna umuhimu wa kutoa ratiba ya mapema na sio kuchelewa kutoa ratiba ya Viwanja. 

Amesema hawana tatizo na Dodoma na watatungulia huko mapema kwani wanaiheshimu sana Mbao Fc ila kamwe hawaiogopi na wapo tayari kucheza hata wangepangiwa kiwanja chochote.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com