Simba SC imekanusha taarifa inayosambazwa ikimtaja Rais wao

Siku moja baada ya tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kufanyika na kutoa zawadi kwa wahusika huku timu ya Simba ambayo ni mshindi wa pili kutokuwepo wala kutuma muhusika katika eneo la tukio ikihisiwa kuwa ni muendelezo wa kugomea zawadi ya mshindi wa pili.
Leo May 25 2017 ziliripotiwa habari za uongo katika mitandao ya kijamii kuwa wekundu wa Msimbazi Simba kupitia kwa Rais wao Evans Aveva wamekubali nafasi ya mshindi wa pili na kufuta malalamiko yao FIFA kuhusiana na TFF kuituhumu kutotenda haki.
Uongozi wa Simba SC kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii zimekanusha taarifa hii iliyokuwa inasambaa mtandaoni 


Simba imekanusha taarifa hizo kupitia ukurasa wao wa instagram “Wanachama, wapenzi na mashabiki wa Simba Sports Club tunawaomba mpuuze ujumbe huu unaosambazwa. Uongozi wa Simba haujatoa taarifa hii”


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com