Sakata la uvamizi: Sirro awataka Clouds kutoa ushirikiano

Kamishna wa Polisi Kanda Maaalum ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema kuwa Jeshi hilo bado lipo kwenye upelelezi kuhusiana na kuvamiwa kwa Clouds Media Group na Mkuu wa Moa wa Dar es Salaam Paul Makonda na pindi upelelezi utakapokamilika hatua zinazotakiwa zitafuata ikiwa ni pamoja na kulifikisha jalada kwa Wakili wa Serikali.
Kamanda Sirro amesema hayo mbele ya wanahabari ambao walihoji hatua ambayo upelelezi huo ulipofikia na namna jambo hilo linavyoshughulikiwa: “Kesi ni ushahidi Kwa hiyo ndugu zetu bado tunapeleleza lakini niwaombe ndugu zetu wa Clouds waendelee kutupa ushirikiano, watupe ushahidi…mimi kazi yangu ni kupeleleza…nikishapeleleza ushahidi uliopo napeleka kwa Wakili wa Serikali.” – Kamanda Sirro.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com