Raia wanne wakigeni wamejeruhiwa kwa kuchomwa na kisu

lukmanRaia Wanne wa Kigeni na Watanzania Wawili wamejeruhiwa kwa kuchomwa na kisu katika Maeneo ya Manispaa ya mji wa Zanzibar.
Akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na  tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Mgharib Hassan Nassir Ali, alisema tukio hilo limetokea jana Jumapili majira ya saa 1 usiku.
Amesema katika tukio hilo Kijana mmoja Mwenye umri wa miaka 25 ambae anafahamika kwa sura alifika kwenye mgahawa wa Lukmaan uliopo Katika Manispaa ya mji wa Zanzibar na kuwachoma visu wageni Watatu waliofika hapo kwa huduma ya chakula.
Akiwataja majeruhi hao amesema ni Mauget Gerarol Mwanamke (66) raia wa Ufaransa ambae amejeruhiwa pembeni ya jicho lake la kulia, Jennifer Wolf Mwanamke (24) raia wa Ujerumani aliejeruhiwa katika sehemu yake ya kichwa na Anna Catharina Ehlgen Mwanamke (20) raia wa Ujerumani aliejeruhiwa Kichwani.
Kamanda Nassir amesema baada ya kijana huyo kufanya tukio hilo alipofika umbali wa mita 60 kutoka eneo la tukio la awali njiani aliendelea kumjeruhi kijana aitwae Hassan  Abdallah Mtanzania Mkaazi wa Kiponda(24) na raia wa Canada Liying Liang kwa kuwachoma kisu mdomoni na shavuni.
Aidha alisema pia kijana huyo alimjeruhi Sajad Hussein mwanaume miaka (55) Muhindi wa Mkunazini ambapo majeruhi hao wote walikimbizwa hospitalli ya Tasakhtaa Global ili kupatiwa matibabu.
Alisema majeruhi hao wote walipatiwa matibabu na kuruhusiwa lakini Mauget Gerarol raia wa ufaransa bado amelazwa hospitalini hapo na anaendelea kupatiwa matibabu.
Aidha kamanda Nassir amesema Jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kumfatilia mtuhumiwa huyo ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria pindipo atapopatikana.
Hata hivyo ametowa wito kwa Wananchi kudumisha amani na utumivu katika maeneo yao ili kulinda hali ya usalama kwa wageni waoitembelea Zanzibar.
Mbali na kauli ya kamanda Nassir kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo bado chanzo cha kijana huyo hakijajulikana kama alitaka kuwapora wageni kutokana na kijana kuwa ni mpungufu wa akili kutokana na kuathirika kwa dawa za kulevya.A
Na:Mwandishi wa zanzibar24.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com