Nape akikanya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambae pia ni Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amekionya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwamba kisipotekeleza ahadi zilizotolewa kwa wananchi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, wanaweza wasiaminiwe tena katika uchaguzi ujao.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter Nape ameandika “Tuliwaahidi na huu ndio mkataba kati ya CCM na Wananchi! Tusipoutekeleza hatutaaminika!”
Tangu alipovuliwa uwaziri, Nape amekuwa akichapisha picha mbalimbali za shughuli alizokuwa akizifanya nchi nzima kuimarisha chama ili wananchi waweze kukiamini kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015.

Nape kwa upande wake amekuwa akisema kuwa sasa ni wakati wa kuwatumikia wananchi wa Mtama walioumuamini na waliokiamini chama chake, kwani asipofanya hivyo kwa kutekeleza ahadi zake, hatoaminiwa tena.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com