Mwenyekiti wa CCM aachiwa kwa dhamana


Iringa. Mahakama ya mkazi mkoa wa Iringa  imemuachia huru kwa dhamana aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu (41) baada ya kukana shtaka linalomkabili.

Akisoma shauri hilo wakili wa Serikali , Alex Mwita alisema Msambatavangu anashtakiwa kwa kosa la kumshambulia Neema Nyongole mnamo Februari 17  mwaka huu maeneo ya Kibwabwa  kinyume na kifungu cha sheria namba 240 cha mwaka 2002.

Baada ya mshtakiwa kusomewa shtaka hilo mahakamani hapo, alikana kutenda kosa hilo na kusema sio kweli.

Wakili Mwita alisema kuwa upelelezi wa shtaka hilo bado unaendelea huku upande wa utetezi ambao unaongozwa na mawakili wawili ambao ni  Alfred Mwakingwe akisaidia na Jackson Chaula waliiomba Mahakama hiyo kumuachia kwa dhamana   kwa sababu kosa linalomkabili mtuhumiwa linaruhusu kupewa dhamana.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com