Mwendesha baiskeli aliyechomwa moto kuzikwa kesho


Mwendesha Baiskeli, Faiza Feruz amefariki kwa kuchomwa moto akiwa nyumbani kwake na mtu anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake mapema wiki hii anatarajia kuzikwa kesho Jumamosi kwenye makaburi ya Njiro, Arusha.


Mwishoni mwa wiki iliyopita mwendesha baiskeli huyo alishika nafasi ya pili katika mbio za baiskeli zilizofanyika mkoani hapa huku nafasi ya kwanza ikienda kwa Abdul Hamis na nafasi ya tatu ikishikwa na Thud Peterson.

Katibu wa chama cha waendesha baiskel Arusha, Andrew Mosses alisema wamepokea kwa masikitiko kifo cha Feruzi kutokana na mchango wake katika chama chao.

Baada ya kusikia jina la mwanamke aliyefariki ndipo tulianza kufuatilia, kwa kuwa tulijua ndiye alikuwa mpenzi wake kwa muda mrefu na mwisho simu zake zikawa zinaita bila kupokelewa na ikabidi tukahakikishe Hospitali kwa kuangalia alama ambazo Marehemu alikuwa nazo akiwa hai ndipo juzi tukagundua alikuwa Faiza Feruzi,ö alisema Mosses.

Tukio la kuchomwa moto watu hao lilitokea Jumatatu wiki hii, awali Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Charles Mkumbo hawakuweza kumtambua mwanaume kutokana na miili waliyoikuta kuwa imeharibika vibaya.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com