Mke na Mume wafariki papo hapo kwa Ajali

Watu wawili wamefariki Dunia papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na gari mapema jana asubuhi katika Eneo la Kianga Rashia wilaya ya Magharibi Unguja.
Tukio hilo lilihusisha gari aina ya Canter yenye namba za usajili Z 717 HD iliyokuwa ikiendeshwa na Amour Salehe Faki (24) likiwa linatokea Dole kuelekea meli sita na lililowagonga Almasi Himid Said (34) na Mkewe Maryam Bakari Juma (30) wakazi wa Kizimbani wakiwa wamepanda Vespa yenye namba za usajili Z 633 DF wakiwa wanatoka Meli sita kuelekea Dole. Bw. Almasi na Mkewe walifariki Dunia papo hapo.
Aidha Canter hiyo pia ilimgonga Nassor Mathias Bruno mkaazi wa Mboriborini Unguja aliyekuwa amepanda Honda yenye namba za usajili Z 909 GN ikiwa pia inaelekea Dole kutokea Meli Sita. Nassor amelazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja akiendelea kupatiwa matibabu.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com