Miss TZ akabidhiwa gari leo, miezi 6 toka achukue taji

Kamati ya Miss Tanzania Alhamisi hii imemkabidhi Miss Tanzania 2016/17 Diana Edward zawadi ya gari lake aina ya Suzuki Swift ikiwa ni miezi 6 toka atangazwe mshindi huko mkoani Mwanza.

Gari ambayo amekabidhiwa Miss Tanzania leo
Mrembo huyo ambaye aliahidiwa kupewa Toyota IST, amekabidhiwa gari hilo nje ya jengo la City Mall Jijini Dar es salaam.
Akiongea na Bongo5 muda mchache baada ya kukabidhiwa gari hilo, Diana ameishukuru kamati hiyo huku akiitaka kujipanga zaidi katika namna ya kuliendesha shindalo hilo.
“Kiukweli sina cha kuongea zaidi ya kuishukuru kamati ya Miss Tanzania maana nimeangaika sana. Mimi sitaki kujua gari ametoa nani, nachojua gari yangu nimekabidhiwa baada ya kuangaika sana,” alisema Diana.
Aliongeza, “Kingine kuhusu kichotokea ningeitaka kamati ya Miss Tanzania wajipange sana, haya mambo hayapendezi, tena yanafanya haya mashindano kuonekana hayana maana,”
Mrembo huyo aliiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo duniani (Miss World 2016) yaliyofanyika huko Marekani.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com