Mh. Salma Kikwete akataa wanaopata mimba kurudi shule

Mke wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Salma Kikwete amesema hakubaliani na suala la wanafunzi kupata mimba na kurudi shule tena kutokana na mazingira yaliyopo.

Mama Salma Kikwete
Akizungumza bungeni leo, Mama Salma amesemaa suala la mimba ni tatizo na suala la utoro ni tatizo pia, ila wao kama wanawake wanawapenda sana na ni lengo lao wabunge wanawake kuwatetea watoto wa kike na mwanamke yeyote yule ambaye yuko katika nafasi ya uongozi.
“Lakini kwenye suala hili la mimba, hasa mimba za utotoni mimi sikubaliani nalo kwamba wakipata mimba warudi tena shuleni. Hilo sikubaliana nalo hata kidogo na sababu ya kutokubaliana nalo ni hizi zifuatazo, kwanza tunazungumzia suala la mila, desturi, utamaduni, na mazingira,” amesema Salma Kikwete.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com