Mchungaji Aliwa na Mamba wakati akitembea Juu ya Maji Kama YESU

Mchungaji wa kijiji kimoja huko zimbabwe Pastor Jonathan Mthethwa ametafunwa vizuri na mamba watatu alipokuwa akijitutumua kutembea juu ya maji Kama yesu katika mto MPUMALANGA au kwa jina maarufu MTO MAMBA kutokana na wingi wa mamba katika mto huo.

Alikuwa anafanya majaribio ya imani(DEMO) aliyowafundisha waumini wake kanisani....

Shemasi aliyehojiwa anashangaa kwa nini aliliwa maana kabla alifunga na kuomba wiki nzima...

Mashuhuda wanasema alitembea ndani ya maji kama mita 30, alipotaka kuanza kupanda ili aanze kutembea juu ya uso wa maji ndipo yalitokea mamamba makubwa matatu na kumtafuta na kumkatata vipande huku mwili wote ukiishia kwenye matumbo ya watafunaji hao...

Waumini Muwe makini na Wachungaji wenu, Leo kaenda yeye kesho anaweza kuibuka mwingine TZ akawaambia kanisa zima litembee juu ya mto ruvu ile sehemu yenye mamba na viboko wengi kama mazoezi ya Imani. Au kama mafunzo ya vitendo baada ya kufundishwa Theory/Nadharia za kiimani kanisani...

Imani na Akili lazima ziende sanjari na Vyote viwe mubashara Muda wote ukikoswa kimoja utaishia kuliwa kama sio wewe basi pesa zako...


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com