Mashindano ya ngumi ya Mstahiki Meya wa Jiji la DSM Mwita yamalizika

NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MASHINDANO ya ngumi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita yamemalizika jana na Timu ya JKT Makao Makuu kuibuka mabingwa wa kombe hilo ikiwa ni kwa Mara ya nne mfululizo.

Mashindano hayo ambayo yalikuwa na mvuto wa Pekee , yalifika tamati hiyo jana na kufungwa na Mbunge wa jimbo la Temeke Abdala Mtolea kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ambaye ndio mdhamini Mkuu wa mashindano hayo.

Timu ya JKT iliibuka mshindi wa mashindano hayo kufuatia wachezaji wake kupata medali nne za dhahabu , huku Timu ya Magereza ikipata medali mbili, Kigamboni medali moja na Mombasa medali moja.

Akizungumza mara baada ya kutoa zawadi kwa washindi , Mbunge Mtolea alimpongeza Mstahiki Meya wa jiji kwa kuandaa mashindano hayo na kusema kuwa ni mchezo ambao unamashabiki wengi na kwamba amewatendea haki wananchi wa jiji lake ambao wanapenda mchezo huo.

Alisema kuwa uwepo wa mashindano hayo umewezesha kuwakutanisha vijana pamoja kutoka sehemu mbalimbali na hivyo itachangia zaidi katika uhamasishaji wa kujiepusha na matukio ya kiuhalifu, makundi mabaya kama vijana.

Alisema lich ya changamoto zilizopo kwenye mashindano hayo lakini wachezaji waliweza kujitoa sambamba na waamuzi wa mchezo huo na hivyo kutumia nafasi hiyo kuwapongeza na kuahidi kushugulikia changamoto zilizopo.

Aliongeza kuwa wapovijana ambao walitamani kushiriki kwemye mashindano hayo lakini kutokana na changamoto mbalimbali walishindwa na kwamba kwenye maandalizi yajayo yatafanyika mapema ikiwa ni kuanzia kwenye ngazi ya kata, Halmashauri na hivyo kufikia tamati ya mchezo huo kwa ngazi ya jiji.

Aidha alisema kuwa baada ya kumalizika kwa mashindano hayo , na kufanyika kwa tathimini , ripoti hiyo itatumika kwenye mandalizi ya mashindano yajayo ambapo itatumika kwa kutumia mapendekezo ya wasimamizi wa mchezo huo sambamba na walimu.

" Mchezo huu unamashabiki wengi, najua wapo ambao walitaka kushiriki lakini kutokana na changamoto za hapa na pale mmeshindwa, sasa kwenye mashindano yatakayokuja, tutawafikia hadi kwenye kata zenu mnapotoka" alisema Mtolea kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Jiji.

Mbunge Mtolea alisema" sasa haya ambayo nimetoka kuyazungumza ni maneno ya mstahiki Meya wa jiji, lakini ninachokwenda kuwaeleza hivi sasa ni maneno yangu, nitamuunga mkono mstahiki kwenye mashindano haya, nitazungumza nae ili mwakani tuanze maandaizi haya mapema" alisema Mbunge Mtolea.
Image may contain: 4 people, people sitting, table and indoorImage may contain: 4 people, people standingImage may contain: 13 people, people smiling, people sitting, shoes and outdoorImage may contain: 1 person, playing a sportImage may contain: one or more peopleImage may contain: one or more people


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com