Mama aliyemuuwa mwanawe naye afariki kwa Kutatanisha

Mwanamke aliyekuwa akishikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake katika kijiji cha wingwi micheweni pemba  naye amefariki dunia  huku polisi na hospitali wakitupiana mpira kuhusu mazingira ya kifo chake.
Jeshi la polisi ambao walikuwa wakimshikilia mwanamke huyo wamesema alifariki akiwa hospitalini  lakini madaktari wamesema walipompokea  mwanamke huyo kutoka kwa polisi akiwa tayari amefariki dunia.
Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini pemba Haji Khamisi Haji  amesema waliamua kumpeleka hospitali mwanamke huyo baada kusema amebanwa na mafua ili ende kupatiwa matibabu .
Daktari aliyemfanyia uchunguzi marehemu huyo khalifan Said Salum  amesema wamempokea mwanamke huyo kutoka kwa jeshi la polisi  akiwa tayari  ameshafariki dunia.
Amesema wakati anaendelea kumpima  marehemu huyo walimkuta akiwa ametokwa na povu jingi mdomoni na hivyo kuchukuwa sampuli kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi akiwa anatoka katika hospitali ya micheweni  amemuona mtuhumiwa wa pili wa tukio hilo akiwa   anapelekwa hospitali kwa kupatiwa matibabu akiwa na ulinzi kutoka jeshi la polisi.
Marehemu pamoja na Watuhumiwa wenzake wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumchinja Mtoto wao mchanga kama ilivyoripotiwa kwenye habari


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com