Makamu wa Rais Kuogoza uombelezaji na ibada ya kuuga miili ya wanafunzi 32 Arusha

Makamu wa Rais, Samia Suluhu kesho saa mbili asubuhi ataongoza wakazi wa Arusha katika Uwanja wa Sheikh Abeid Karume kuaga miili ya wanafunzi 32 waliofariki katika ajali ya gari ambapo serikali imegharamia sanda  na majeneza kwa wanafunzi wa shule Lucky Vincent waliopoteza maisha jana kwenye ajali.

Akitoa taarifa hiyo leo Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro,  amesema taarifa za awali zinaonyesha tayari serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda za kuhifadhia miili ya marehemu ambao kesho wanatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Aidha Lazaro amesema viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri na wabunge bado wanaendelea kukusanyika katika eneo la shule ya Lucky Vincent  kwa ajili ya kikao.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com