Majeruhi wa ajali ya basi Karatu wawasili Marekani

Majeruhi watatu wa ajali ya basi iliyotokea huko Karatu wiki mbili zilizopita na kusababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1, huku ikiacha majeruhi hao watatu ambao mpaka juzi walikua wakipata matibau katika hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru kabla ya kusafirishwa kupelekwa Marekani.

Taarifa tulioipata hivi sasa kutoka kwa Mbunge wa Singida Kaskazini Mhe. Lazaro Nyalandu amesema kuwa Ndege iliyowachukua watoto hao majeruhi kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana asubuhi  imewasili Mjini Charlotte NC, nchini Marekani saa Moja iliyopita.
Watoto hao wamepelekwa Moja kwa Moja hospital kuu mjini Charlotte kwa ajili ya kuimarishwa kiafya (medical stabilisation), na baadae watachukuliwa kwa ndege nyingine maalumu (air ambulance) kuelekea hospitali ya Mercy, Iliyopo Sioux City, katika Jimbo la Iowa kwa huduma kamili za matibabu.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com