Majeruhi huyu wa ujambazi asimulia alivyojeruhiwa

Majeruhi wa tukio la ujambazi lililotokea juzi usiku jijini Dar es Saalam, Zacharia Sijaha ameeleza namna alivyojeruhiwa na kupelekwa na polisi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.

Sijaha alisema kuwa muda mfupi baada ya majambazi hao kuvamia na kupiga risasi hewani, polisi walijibu mapigo hayo kwa kuanzisha mapambano. 

“Nilikuwa kwenye biashara ya chipsi nje ya duka, ghafla nikaowaona watu wakishuka kwenye pikipiki, walizungumza kwa muda kidogo, lakini mazungumzo yao yalikuwa kama wanabishana,” alisema.


Aliongeza kuwa baada ya muda watu hao walishuka na kupiga risasi mbili hewani na kuwaamuru watu waliokuwa eneo hilo walale chini. 

“Kumbe polisi nao walikuwepo nao wakajibu risasi hizo na kuwashambulia majambazi wale, nikiwa chini nimepigwa taharuki risasi ziliendelea kusikika ghafla moja ikanipata kwenye mguu wa kulia,” alisema.


Alisema baada ya kumalizika mapambano hayo polisi walimchukua wakampeleka Muhimbili, lakini baada ya kufanyiwa vipimo ikaonekana risasi haikuingia kwenye mfupa.

Chanzo: Mwananchi

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com