Maiti za wahamiaji haramu Zaokotwa Mto Ruvuma


Raia wanane kutoka Ethiopia wamekutwa wakiwa wamefariki na miili yao kutupwa katika makaburi ya kijiji cha Amani Makolo tarafa ya Kingonsera wilayani mbinga mkoani wa Ruvuma

Kaimu kamanda wa polisi ACP Dismasi Kisusi amesema kuwa raia hao wa Ethiopia walikuwa wanasafirishwa kwenda nchi ya Africa ya kusini kupitia ziwa Nyasa Upande wa nchi jirani ya ya Malawi.

Vifo vya Waithiopia hao vinatokana na kubebwa kwenye kontena la lori wakitokea mpaka wa Namanga Arusha hivyo kutokana na hali mbaya ya hewa hali zao zilianza kubadilika na kupelekea vifafo vya watu nane na wengine 25 wamenusurika ambapo wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali.

Jeshi la polisi mkoa wa ruvuma kwa kushirikiana na jeshi la uhamiaji linaendelea na uchunguzi kubaini walioleta miili ya marehemu na wale wasiliokamatwa hatua za kisheria zitafuatwa.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com