Kutoka Ofisini kwa Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli  amemkaribisha  ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma,  tukio lililofanyika jana siku ya Alhamisi. Ofisi ya Mama Janeth Magufuli  kupitia ofisi yake inaendesha shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu walioathirika na ugonjwa wa Ukoma .
 Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma,  wakielekea kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akimsindikiza Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma, aliyemtembelea kwenye  ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma, kwenye ofisi yake Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha matarumbeta cha Usambara kikiwakaribisha Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) na  Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele, Zuma alipomkaribisha mgeni wake huyo kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
PICHA NA IKULU


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com