Kuhusu Mkuu wa Mkoa aliyefariki Dunia

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amefariki dunia JANA saa nne asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Mdogo wa marehemu, Shaibu Mwambungu amesema kaka yake alifariki dunia JANA asubuhi baada ya hali yake kubadilika ghafla akiwa hospitalini hapo.

Shaib amesema taratibu za mazishi zitatolewa baadaye ambapo kwa sasa anajiandaa kusafiri kutoka Songea kuja jijini Dar es salam kwa ajili ya mazishi.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com