Kufuru: Utajiri wa Kutisha wa Mhasibu Mkuu wa TAKUKURU

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeweka wazi mali za aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Godfrey Gugai, ambaye utajiri wake unakadiriwa kuwa na thamani ya Shilingi bilioni 3.5.
Hatua hiyo imekuja kufuatia ombi la Mkurugenzi wa mashtaka DPP aliloliwasilisha katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu kuweka zuio la mali hizo.
Bw. Gugai anatarajiwa kufikishwa mahakama siku za hivi karibuni kwa makosa ya rushwa au makosa yanayofanana na rushwa.
Miongoni mwa mali zilizotajwa kumilikiwa na Bw. Gugai na ambazo zimezuiwa kwasasa ni kama ifuatavyo:
  • Viwanja 33
  • Nyumba 7 za ghorofa moja
  • Nyumba 8 za kawaida
  • Magari 5
  • Pikipiki 1

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com