Kizimbani kwa kumpiga mke mwenziwe

Jeshi la polisi mkoa waKaskazi Pemba limemfikisha mahakamani mtuhumiwa DawaSuleiman Khamis (37) mkaazi wa Miti ulaya Wete kwa madai ya kumpiga mke mwenziwe na kumsababishia maumivu makali
Imedaiwa mahakamani hapo kuwa siku ya tarehe 20/4 2015 huko Kipangani wete mtuhumiwa huyo alimpiga kwa magongo Hadia Mohd ambae ni mke mwenziwe  na kusababishia maumivu kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Mtuhumiwa huyo amba anakabiliwa na mashtaka mawili la mwanzo lakumpiga mke mwenziwe pamoja na la kuharibu mali aliiomba mahakama impe dhamana jambo ambalo lilikubali mahakamani hapo na kuachiwa baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com