Jela miaka miwili kwa kumdhalilisha mtoto wa miaka minne

Mahakama ya Wilaya ya Mwera imemuhukumu kutumikia chuo cha mafunzo miaka 2 mstakiwa Ali Juma Ali (22) mkaazi wa Mtopepo kwa kosa la kumkashifu mtoto wa miaka minne jina limehidhiwa.
Mnamo tarehe 20/02 mwaka jana majira ya saa 9 mchana huko mtopepo mshtakiwa huyo alimvua nguo za ndani mtoto huyo na kumfanyia vitendo vya kumkashifu jambo ambalo ni kosa kisheria.
Sambamba na hukumu hiyo pia mahakama ilimtaka mshtakiwa huyo kulipa fidia ya shilingi laki 5 ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hiyo.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com